Posted by Williammalecela.com on Thursday, October 06, 2016
 |
Mkuu Wa
Wilaya Ya Kinondoni Mh Ally Hapi Leo ametembelea miradi mikubwa ya maji
inayosimamiwa na Dawasco na kusambaza maji maeneo mbalimbali ya jiji
ikiwemo wilaya ya Kinondoni.
Katika ziara hiyo iliyoongpzwa na
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mkuu wa wilaya ya kinondoni ameambatana
na Mtendaji Mkuu Wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na wakuu wa
wilaya za Kibaha,Bagamoyo,Temeke,Kigamboni na Ilala ambao wote wilaya zao zinahidumiwa na miradi ya maji ya DAWASCO.
Katika hatua hiyo Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Na Wakuu Wa Wilaya
Zingine Wakiongozwa na Mhandisi Cyprian Luhemeja wameweza kutembelea
kituo cha Dawasco Magomeni,kituo cha Dawasco Kibaha,Mtambo wa Maji wa
Ruvu Juu(Mlandizi) pamoja na Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini(Bagamoyo) |
0 comments:
Post a Comment