Taswira kutoka eneo la ajali.
MSANII
wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Endless Fame inayomilikiwa na malkia wa
filamu Bongo, Wema Sepetu, Mirror amepata ajali maeneo ya Ununio jijini
Dar hivi punde.
Inasemekana,
Mirror alikuwa akielekea nyumbani kwa bosi wake, Wema ‘Madam’ na baada
ya kufika maeneo hayo alipata ajali mbaya iliyosababisha gari alilokuwa
nalo, (gari ndogo aina ya Toyota lenye namba T 169 DDK) kutumbukia
katika mtaro.
Msanii Mirror.
Inasemekana
Mirror alikuwa peke yake ambapo baada ya ajali alipata maumivu makali
maeneo ya miguuuni na hapohapo alipopigiwa simu Wema hakupatikana hewani
na alipopigiwa Kadinda iliita bila kupokelewa.
Hata hivyo wasamaria wema wamemchukuwa na kumuwaisha hospitali kwa matibabu zaidi.
Kwa habari zaidi ya kitakachoendelea tutazidi kuwajuza, endelea kufuatilia mtandao huu…
0 comments:
Post a Comment