,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, April 7, 2017

Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, amesema atamshtaki yeyote atakayetaka kupata jina kubwa kwa jamii kupitia mgongo wa jina lake kama baadhi ya wasanii waliotambulika kwa jamii kupitia jina lake.

Wema alidai baadhi ya wasanii waliopata majina makubwa kutokana na kuwa karibu naye hawana heshima wala fadhila kwake, hivyo hataki kurudia makosa aliyowahi kuyafanya ya kumwamini kila mtu bila kujua malengo yao.
Akiongea na Gazeti la Mtanzania wiki hii, Wema alisema, “Kwa sasa najielewa tofauti na zamani hivyo sitaki niwe daraja la kuwatangaza watu na kuwapatia umaarufu kupitia jina langu,”.
Mbali na hilo, Wema amekava jarida kubwa la True Love Magazine East Africa la nchini Kenya. Kwa sasa jarida hilo linaingia mtaani katika msimu huu wa pasaka. Kwa mujibu wa taarifa, katika jarida hilo Wema amezungumzia hela, wanaume pamoja na maisha yake kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi