Jeshi la polisi nchini Uingereza limesema kwamba mwanaume aliyehusika katika shambulio la kigaidi katika eneo la Westminister kuwa ni Khalid Masood, kwa mujibu wa taarifa walizopewa na wapelelezi wa
Scotland Yard.
Wapelelezi hao wamesema kwamba Masood anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 52 alizaliwa katika
eneo la Kent na wapelelezi wanaamini kwamba alikuwa akiishi Midlands
magharibi.
Hatahivyo, alitambuliwa na polisi
na kwamba alikuwa ameshtakiwa kwa kushambulia watu ikiwemo umiliki wa
silaha na kusababisha taharuki mbele ya uma.
Watu saba wamekamatwa katika
uvamizi mjini London na Birminghamkufuatia shambulio la Westminster
lililowauwa watu wanne, kwa mujibu wa polisi.
Mamia ya polisi wa
upelelelezi wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha wakifanya uchunguzi
dhidi ya makazi sita, amesema kaimu naibu wa kamishna wa polisi Mark
Rowley.
Wale waliokufa walikuwa ni mwanamke mmoja mwenye umri wa
miaka 40, mwanamume mwenye miaka 50 Polisi Keith Palmer pamoja na
mshambuliaji, aliongeza.
Saba miongoni mwa majeruhi bado wako hospitalini katika hali mahututi.
Wengine 29 zaidi wamekuwa wakipata matibabu hospitalini, ameongeza Rowley.
Katika
shambulio la Jumatano, mwanamume mmoja aliendesha gari kwenye njia
ndogo karibu na Westminster na kuwagonga wapitanjia, huku akiwaacha
kadhaa na majeruhi.
Kisha alimdunga kisu polisi na akapigwa risasi na polisi kwenye eneo la bunge.



0 comments:
Post a Comment