Producer Messen Selekta na msanii wa Singeli Man Fongo wamezika beef lao baada ya kutupiana maneno kwa zaidi ya wiki mbili juu ya pesa za tangazo alilotakiwa kufanya Man Fongo.
Kwenye #FridayNiteLive na #Sammisago, Messen amesema ni kweli palikuwa na mchongo wa pesa ila sio milioni 15 kama alivyosema Man Fongo.
Messen anasema “Pesa iliyokuwa tayari kutolewa ilikuwa milioni tatu na mikataba tulikuwa tayari tumesaini ila kutokana na Man Fongo kusita kufanya kazi, tangazo lilichlewa na mchongo ukafutwa”
Pia Man Fongo naye amekiri kuwa pesa alizotaja mapema ‘Milioni 15‘ yeye aliambiwa tu na meneja wake mpya #Wiso na ndio kilicho mfanya asite kufanya mchongo huo kutokana na uelewa wake kuwa dili kama hizo zinakuja na pesa nyingi zaidi….
Aliyekuwa meneja wa Man Fongo #GMaker naye amekiri kuwa dili hilo lilivyokuja kwake aliwaachia Man Fongo na Messen walifanyi wao bila yeye kuhusika jambo ambalo lilipelekea wawili hao kutoelewana.
0 comments:
Post a Comment