Wanandinga wanaounda kikosi cha Serengeti Boys wamekabidhiwa kadi zao za
bima ya afya toka katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF katika makao
makuu ya mfuko huo yaliyopo kurasini jijini dar es Salaam.
Akiwakabidhi
kadi hizo kwa wanandinga hao, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko NHIF Bi Angela Mzirai
amesema kutokana na dhoruba ambazo zimekuwa zikiwakuta wanamichezo wawapo
uwanjani ni vema wanamichezo wakawa na bima ya afya kwani maradhi au majeraha
hujitokeza muda wowote ule.
Angela
amesema NHIF wamefikia katika hatua ya kuwasajili wanandinga wa Serengeti
katika mfuko huo kwani NHIF inthamini sana michezo na pia mfuko huo umetoa
fursa kwa wanandiga hao kutumia chumba cha kufanyia mazoezi kilichopo katika
ofisi za mfuko huo.
Katika hatua nyingine Angela ameipongeza Serengeti
Boys kwa kufanikiwa kupata nafasi ya kwenda kushiriki katika fainali za AFCON
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zinazotaraji kwenda kufanyika nchini
Gabon.
Angela
amesema Serengeti imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya mchezo wa soka nchini
kwani sasa inaliwakilisha vema Taifa na kulitangaza kimataifa.
Nae Meneja Wanachama wa NHIF Elentruda Mbogoro amewataka wanamichezo
katika mbalimbali kujiandikisha katika mfuko huo kuanzia ngazi ya michezo ya
mashule hadi katika ligi mbali mbali.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ameishukuru NHIF kwa
kuwapatia wanandinga hao kadi hizo.
-



0 comments:
Post a Comment