,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, March 17, 2017

Klabu ya soka ya Azam FC imeendelea kujifua kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya klabu ya Mbabane Swalows.


Azam FC inakabiliwa na mchezo huo muhimu utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo, uliopo mjini Mbabane, Swaziland siku ya Jumapili saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kuelekea katika mchezo huo, klabu ya Azam FC inahitaji japo sare kama si ushindi ili ifanikiwe kusonga katika inayofuata katika kombe la Shirikisho barani AFrika CC.


Katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Cahamazi Azam ilipata ushindi wa bao 1-0.

katika hatua nyingine Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mh. Richard Lupembe, ameipigia chapuo klabu ya Azam na kusema kwamba klabu hiyo inawatia moyo Watanzania wanaoishi nje ya nchi.


Balozi Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

“Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza (vs Bidvest) na nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi