Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.
Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.
“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi...Wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Machi, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akielezea changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Maggid Mwanga baada ya kuongea na wanakjijiji wa Fukayosi wilayani humo aliposimama kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.






0 comments:
Post a Comment