Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na
watu wasiojulikana.
Taarifa za awali aimeeleza kwamba tukio hilo limetokea nyumbani kwake Kulambiro, Kisaasi
kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Felix ambae aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu
cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi
walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Wakati huo huo walinzi wake wawili waliokuwa pamoja nae nao wameuawa.

0 comments:
Post a Comment