JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es
Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya
chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo
vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa
maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali
wa chama hicho kwa mujibu wa katiba, haikubaliki.
Viongozi wa vijana wa chama hicho katika wilaya za Temeke, Ilala na
Kinondoni, wakizungumza na waandishi wa habari jana, walimtaka Mtatiro
kuacha kuwakashifu viongozi hao vinginevyo wataomba uongozi kuwachukulia
hatua kulingana na Katiba ya chama ikiwemo kuondolewa uanachama.
Akisoma taarifa ya upotoshaji unaofanywa na wanaojiita Kamati ya
Uongozi wa chama hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho
wilaya ya Ilala, Canal Shughuly, alisema Katiba ya chana hicho inaamini
kwamba kila mtu ana wajibu wa kuheshimu utu, uhuru na haki za wengine
pamoja na kutii sheria halali za nchi.
Shughuly aliongozana na Katibu wa Vijana wa chama hicho Ilala, Abdul
Komesha na Katibu wa Kinondoni, Yusuph Kitogota alisema kitendo cha
kubezwa kwa msajili pamoja na maamuzi yake wakati anatambulika kikatiba
ni kuonesha jinsi alivyo mbumbumbu wa kuielewa katiba ya chama
anachokiamini.
Alisema Mtatiro ni miongoni mwa vijana waliopata bahati ya kushika
nafasi ya juu ya uongozi wa ndani ya CUF ya Naibu Katibu Mkuu bara
ambayo aliteuliwa na Lipumba, lakini uteuzi huo ulitenguliwa baada ya
kukubwa na kashfa ya ubadhirifu wa Sh milioni 86 kwa ajili ya ununuzi wa
bendera na vifaa vingine vya chama.
0 comments:
Post a Comment