
Mashabiki wa
muziki wa bongo fleva wamemjia juu msanii Harmonize wakimtuhumu kumuiga
Diamond Platnumz, kwenye kazi zake hadi mavazi.
Malalamiko hayo
yamezidi kushamiri baada ya msanii Dully Sykes kuachia video ya Inde
aliyomshirikisha Harmonize, ndipo mashabiki kuamua kutoa yao ya moyoni,
baada ya kuona jinsi alivyokuwa akicheza mpaka uimbaji wake, na kumtaka
awe mbunifu kwa mitindo yake mwenyewe.
"Harmonize try to do your
Own Style at LIST Don't copy everything from Diamond even ya in Same WSF
at Least Do your Style to Inspire your fans, but still love you",...
aliandika shabiki aliyejulikana kwa jina la Nadia Nadia.
"Harmonize anakopi kila kitu kwa Diamond. Inachosha".....aliandika shabiki mwengine Kennedy Daima Mmari.
Naye
Ruth Murira aliandika....."Hermonize pliz try to do it ur own way,
styles ni za Mondi, kavalia pia ka Diamond, for a moment i thought its
Diamond,aaaaish".
Tatizo hili si mara ya kwanza
kujitokeza kwa msanii huyo, huku wengi wakisema kuwa chini ya Diamond
haina maana aige kila kitu kutoka kwake, hata kama ndiye mtu
anayemuangalia kisanaa (role model), kwani kwa kufanya hivyo atakuwa
anaficha kile alichonache yeye kama Harmonize, na kuuvaa u-Diamond.
0 comments:
Post a Comment