Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi
DIVA
mwenye ‘title’ kubwa Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa tangu awe mzazi
anajitahidi kuishi maisha ya kistaarabu sana kiasi kwamba hahitaji kuwa
na skendo ili kuitunza heshima yake kwa mwanaye wa kiume aitwaye Terry
pale ambapo atakuwa kijana.
Shamsa
alisema hayo wakati akipiga stori mbili-tatu na gazeti hili,
alipoulizwa kwa nini anapendelea kuvaa mavazi mafupi alisema kuwa hiyo
ni ‘hobby’ yake tangu utotoni, kila mmoja kwenye familia yake anafahamu
hilo na wala haihusiani kabisa na malezi ya mtoto.
“Mimi
nililelewa na mama yangu mkubwa ambaye ameolewa na Mzungu, tangu
udogoni alikuwa ananivalisha nguo fupi pamoja na watoto wake. Kwenye
familia yetu suala hilo si tatizo wala halihusiani na malezi ya mtoto,
ninaimani hata Terry akikua ataliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa,”
alisema Shamsa.
0 comments:
Post a Comment