,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, June 18, 2016

NitoANDREW CARLOS, IJUMAA
 Msanii wa kike wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anasumbua na wimbo wake wa One More Night, Hadija Maige ‘Kadja Nito’ anadaiwa kupigwa ndoa ya fasta siku chache baada ya Mfungo wa Ramadhani kuanza.

Chanzo ambacho ni rafiki wa msanii huyo  kilitung’ata sikio kuwa, Kadja ambaye ni mama wa mtoto mmoja alikuwa na jamaa yake ambaye alimuomba amuoe kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili akampikie futari, mambo yakaenda sawa na ndoa  ikafungwa kimyakimya.
Baada ya kunasa ubuyu huo, paparazi wetu alimvutia waya Kadja na kumuuliza kuhusu jambo hilo la heri ambapo alifunguka: “Mmh! Yaani ninyi bwana, mimi siyo wa kuolewa ndoa ya futari, halafu nachukia sana kufuatiliwa mambo yangu binafsi.
“Mambo ya ndoa sasa hivi yanakujaje, wewe niulize nina wimbo gani mpya, naendeleaje na swaumu, hapo sawa.”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi