BAADA
ya kushikiliwa katika Gereza la Makala mjini Kishansa kwa zaidi ya siku
saba, mkongwe wa muziki wa Kilingala, Koffi Olomide ‘Grand Mopao’
hatimaye ameachiwa huru na anatarajiwa kupiga bonge moja la shoo ya bure
leo mjini Kinshasa.Kwa
mujibu wa chanzo, Koffi aliyewekwa ndani baada ya kusambaa kipande cha
video akimpiga teke moja kati ya madensa wake aliyetambulika kama
Pamela, leo atafanya shoo ya bure katika Uwanja wa Veledrome uliopo
Kinshasa.
“Atafanya
shoo ya bure kabisa bila kiingilio katika uwanja wa siku nyingi wa
Veledrome kisha kesho atafanya shoo nyingine ndani ya Invest Hotel mjini
Kinshasa ambapo shoo hii ya pili ambayo ni kesho itakuwa kwa kiingilio
na siyo bure,” kilisema chanzo hicho.
Mara ya mwisho kabla ya kuachiwa huru, mwanasheria wa Koffi alisema;
“Ni
aibu. Ni lazima afurahie haki zake. Mahakama zetu zina kasoro kwa
makosa yaliyofanyika nje ya nchi, hasa kwenye kesi hii. Koffi anajua
ukubwa wa matendo yake na aliomba msamaha na ataachiwa huru hivi
karibuni,” alisema mwanasheria huyo anayetambulika kama Master Lukoo
Ruffin.
Mwishoni
mwa mwezi uliopita, Koffi alijikuta matatani baada ya kumpiga teke
Pamela muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Polisi
wa Kenya walimkamata usiku huo na kumrudisha kwao Kinshasa hali
iliyopelekea kuvunjika kwa shoo aliyokuwa amepanga kufanya.
Alipofika
nchini kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika mji wa
Kinshasa, akiwa nyumbani kwake, polisi walimvamia na kumpeleka
mahakamani.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
0 comments:
Post a Comment