
MCHEKESHAJI maarufu, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ amejitumbukiza kwenye siasa kwa kugombea ubunge jimbo la Kisarawe kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF). Akizungumza na Saluti5 jijini Dar es Salaam, Kingwendu alisema kuwa hivi sasa yuko katika mchakato wa kusubiri matokeo ya kura za maoni ambapo hata hivyo ana imani atapita kwa kishindo.
Kingwendu alisema kuwa, endapo atafanikiwa kupita katika uchaguzi huo, atahakikisha anatatua kero zote za wakazi wa Kisarawe zilizoshindwa na viongozi waliotangulia.
0 comments:
Post a Comment