Posted by Williammalecela.com on Wednesday, April 27, 2016
Huyu ndiye Verkys Kiamungana Wazela Mbongo Mateta, Mwanamuziki maarufu sana aliyewahi kuitikisa Africa nzima akiwa na kundi la Orch. Veve huku pia akimiliki makundi ya bendi za Orch. Lipua Lipua, Orch. Kamale, Orch. Kiam na Orch. Veve International. Verkys alianza safari yake ya Muzki kwenye bendi ya TP. Ok Jazz ya Mzee Lwambo Makiadi na siku moja wakiwa safarini Paris/France Verkys aliamua kujitoa bendi ya Mkongwe huyo Marehemu na kuanzisha bendi yake mpya ya Orch. Veve ilikuwa ni Mwaka 1972 na huu wimbo wa "Nakomintunaka" ndio uliokuwa wimbo wake wa kwanza kuutunga na kuurekodi ukiwa na maana ya kiswahili kwamba "Kwanini Wazungu wanatenegeneza kila kitu kibaya kuwa nu cheusi na hata Yesu ni lazima alikuwa Mzungu?". Verkys ambaye alikuwa akifahamika kwa majina yake ya KIAMUANGANA WAZELA MBONGO MATETA yupo mpaka leo anaishi mjini Kinshasa na pamoja na kustaafu kupiga muziki sasa anamiliki Studio kubwa nchini humo za kurekodi miziki na kwamba 60% ya muziki unaorekodiwa nchini humo unakuwa na hisa zake.
0 comments:
Post a Comment