Wanajeshi wa Iraq walionekana wakiukimbia mji wa Ramadi wakiziacha
silaha zao na magari yasiyoweza kutobolewa na risasi, katika kile
kinachoonekana kuwa pigo kubwa l
a kushindwa vita dhidi ya Dola la Kiislamu licha ya ongezeko la mashambulizi ya kutokea angani dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.
Maiti zilionekana zimezagaa katika barabara za mji huo, baadhi zikiwa zimechomwa moto, huku maafisa wakiripoti kwamba wanamgambo wa kundi hilo walifanya mauaji ya kiholela ya wanajeshi wa Iraq na raia.
"Mji wa Ramadi umeanguka. Mji umedhibitiwa kabisa na jeshi linakimbia," alisema Muhannad Haimour, msemaji wa gavana wa mkoa wa Anbar.
"Tunakaribisha kundi lolote wakiwemo waasi wa kishia, waje watusaidie kuukomboa mji wetu kutoka mikononi mwa wanamgambo. Kilichotokea leo ni hasara kubwa iliyosababishwa na jeshi kushindwa kujipanga vizuri," alisema Naeem al Gououd, kiongozi wa ukoo wa madhehebu ya Sunni wakati alipozungumza na shirika la habari la Associated Press.
Mwanamume wa Kisunni akimsukuma mama mlemavu nje ya Baghdad
Gavana wa mkoa wa Anbar, Suhaib al Rawi, alisema anadhani harakati ya
kijeshi inayofanywa na jeshi la Marekani ni hatua nzuri ya kuelekea
kulishinda kundi la Dola la Kiislamu. "Operesheni yoyote ya maana
inayofanywa na vikosi vya muungano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu
itakuwa na matokeo mazuri. Kundi hili halitishii tu usalama wa Iraq na
Syria bali pia usalama wa ulimwengu mzima. Tunahitaji operesheni za
namna hii, zinazotoa ishara kwamba muungano wa kimataifa umejizatiti
kuyashinda makundi ya kigaidi yanayotishia sio tu mkoa wa Anbar, Iraq na
Syria bali dunia nzima."
Wakaazi wakimbia Ramadi
Mamia ya wakazi wa Ramadi waliukimbia mji huo siku ya Jumamosi wakihofia mashambulizi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu lakini wakanyimwa ruhusa ya kuingia Baghdad na mikoa mingine na wanajeshi wa Iraq kwa sababu za kiusalama. Wakazi hao sasa wamekwama karibu na daraja la Bzibiz, kiasi kilometa 65 kutoka mji mkuu Baghdad na hawaruhusiwi kuvuka mto wa Euphrates kuelekea mji huo.
Um Mohammed, ambaye ni miongoni mwa wakaazi waliokwama, alisema hali ilikuwa ngumu Ramadi. "Vurugu, machafuko na hofu vimeenea katika barabara za Ramadi. Makombora na mabomu yalianguka kiholela kwa nyumba. Kuna ripoti mpya kwamba familia nyingi zimeuwawa. Wanawake walionekana wakikimbia mabarabarani."
Wakimbizi wa Iraq mkoani Anbar
Huku akikaribia kushindwa, waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi,
aliamuru wanajeshi wasiondoke maeneo yao katika maeneo yote ya mkoa wa
Anbar, akihofia wapiganaji wanaweza kuliteka eneo zima la jangwa
lilishohudia mapigano makali baada ya uvamizi wa Iraq mnamo mwaka 2003
ulioongozwa na Marekani ambao ulimuangusha kiongozi wa zamani wa Iraq,
hayati Saddam Hussein.
Marekani yafuatilia matukio ya Ramadi
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema inaendelea kufuatilia ripoti za mapigano yanayoendelea mjini humo, huku ikikiri wanamgambo wa kundi hilo wanaonekana kuwa na nguvu zaidi katika makabiliano yanayoendelea. Msemaji wa wizara hiyo Maureen Schumann amesema ni mapema mno kutoa kauli kuthibitisha kinachoendelea Ramadi kwa sasa, lakini hata kama mji huo utaanguka mikononi mwa Dola la Kiislamu, muungano unaoongozwa na Marekani utawasaidia wanajeshi wa Iraq kuukomboa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alisema bado ana imani na vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu. Akiwa katika ziara nchini Korea Kusini, Kerry amesisitiza vita dhidi ya kundi hilo vitakuwa vigumu na virefu katika mkoa wa Anbar, ambako wanajeshi wa Iraq hawajakuwa imara.
Makundi ya waasi wa Kishia yamekusanyika mjini Ramadi mapema leo kuvisaidia vikosi vya Iraq kujaribu kuukomboa mji wa Ramadi.
a kushindwa vita dhidi ya Dola la Kiislamu licha ya ongezeko la mashambulizi ya kutokea angani dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.
Maiti zilionekana zimezagaa katika barabara za mji huo, baadhi zikiwa zimechomwa moto, huku maafisa wakiripoti kwamba wanamgambo wa kundi hilo walifanya mauaji ya kiholela ya wanajeshi wa Iraq na raia.
"Mji wa Ramadi umeanguka. Mji umedhibitiwa kabisa na jeshi linakimbia," alisema Muhannad Haimour, msemaji wa gavana wa mkoa wa Anbar.
"Tunakaribisha kundi lolote wakiwemo waasi wa kishia, waje watusaidie kuukomboa mji wetu kutoka mikononi mwa wanamgambo. Kilichotokea leo ni hasara kubwa iliyosababishwa na jeshi kushindwa kujipanga vizuri," alisema Naeem al Gououd, kiongozi wa ukoo wa madhehebu ya Sunni wakati alipozungumza na shirika la habari la Associated Press.
Wakaazi wakimbia Ramadi
Mamia ya wakazi wa Ramadi waliukimbia mji huo siku ya Jumamosi wakihofia mashambulizi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu lakini wakanyimwa ruhusa ya kuingia Baghdad na mikoa mingine na wanajeshi wa Iraq kwa sababu za kiusalama. Wakazi hao sasa wamekwama karibu na daraja la Bzibiz, kiasi kilometa 65 kutoka mji mkuu Baghdad na hawaruhusiwi kuvuka mto wa Euphrates kuelekea mji huo.
Um Mohammed, ambaye ni miongoni mwa wakaazi waliokwama, alisema hali ilikuwa ngumu Ramadi. "Vurugu, machafuko na hofu vimeenea katika barabara za Ramadi. Makombora na mabomu yalianguka kiholela kwa nyumba. Kuna ripoti mpya kwamba familia nyingi zimeuwawa. Wanawake walionekana wakikimbia mabarabarani."
Marekani yafuatilia matukio ya Ramadi
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema inaendelea kufuatilia ripoti za mapigano yanayoendelea mjini humo, huku ikikiri wanamgambo wa kundi hilo wanaonekana kuwa na nguvu zaidi katika makabiliano yanayoendelea. Msemaji wa wizara hiyo Maureen Schumann amesema ni mapema mno kutoa kauli kuthibitisha kinachoendelea Ramadi kwa sasa, lakini hata kama mji huo utaanguka mikononi mwa Dola la Kiislamu, muungano unaoongozwa na Marekani utawasaidia wanajeshi wa Iraq kuukomboa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alisema bado ana imani na vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu. Akiwa katika ziara nchini Korea Kusini, Kerry amesisitiza vita dhidi ya kundi hilo vitakuwa vigumu na virefu katika mkoa wa Anbar, ambako wanajeshi wa Iraq hawajakuwa imara.
Makundi ya waasi wa Kishia yamekusanyika mjini Ramadi mapema leo kuvisaidia vikosi vya Iraq kujaribu kuukomboa mji wa Ramadi.

0 comments:
Post a Comment