Marekani inawasaidia raia wake, raia wa Canada na raia wengine wa kigeni kuondoka nchini Burundi kufuatia wiki kadhaa za maandamano na jaribio la mapinduzi lililozimwa. Msemaji wa
wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani Jeff Rathke amesema mbali na Wamarekani wapatao 20 waliosafiri kwa ndege hadi Kigali nchini Rwanda hapo jana, Marekani iliwasaidia raia wanne wa Canada pamoja na raia wa mataifa mengine ya kigeni. Marekani iliufunga ubalozi wake mjini Bujumbura Ijumaa iliyopita. Hapo jana rais wa Burundi Pierre Nkurunzia alijitokeza hadharani kwa mara kwanza tangu jaribio la mapinduzi la Jumatano iliyopita. Katika hotuba yake fupi, kiongozi huyo hakulitaja jaribo hilo la mapinduzi, badala yake alizungumzia vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa al Shabaab wenye ghadhabu na Burundi na nchi nyingine za Afrika kwa kupeleka wanajeshi katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.

0 comments:
Post a Comment