Kwa mara nyingine tena, Uchina
imemlaumu kiongozi wa Tibet aliyeko uhamishoni Dalai Lama, kwa kutokuwa
mwaaminifu na kushinikiza kiujanja uhuru wa watu wa Tibet.
China imeanzisha makabiliano makali dhidi ya kiongozi wa kidini wa watu wa Tibet, Dalai Lama, na kumlaumu kwa kutumia ghasia kushunikiza uhuru wa Tibet.
Kwa muda mrefu Dalai Lama amekuwa akitetea uhuru wa kujitenga wa jimbo la Tibet, na alikuwa na matumaini makubwa kwa Rais wa sasa wa China, Xi Jinping, atatumia mbinu tofauti katika uhusiano naye na wa watu wa Tibet.
Taarifa hiyo pia ambayo ilichapishwa na shirika la habari la kitaifa la Xinhua, inasema kuwa wakuu mjini Beijing wanamuomba Dalai Lama kuweka kando ndoto yake ya hatma ya baadaye ya Tibet.

0 comments:
Post a Comment