,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, March 9, 2017


Wasanii mbalimbali wanaochipukia katika sanaa ya uigizaji nchini wamejitokeza katika usaili uliofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kutafuta fursa ya kushiriki katika Tamthilia ya WHO CHEAT.


Blogu ya Jamii imeshuhudia mamia ya wasanii waliojitokeza kushiriki katika usaili huo ulioandaliwa na Ndauka Advert kwa ushirikiano na Afrika Swahili TV.

Katika Usaili huo msanii na muigizaji wa filamu nchini Rose Ndauka amesema amefurahishwa na kuridhishwa na vipaji vilivyojitokeza.

Ndauka amesema wasanii waliojitokeza wameonyesha vipaji vya hali ya juu hivyo anaamini atapata waigizaji wazuri na watakaoleta chachu katika tamthilia hiyo.

Nao baadhi ya wasanii waliojitokeza ili kuwania nafasi ya kushiriki katika tamthilia hiyo wameahidi kuhakikisha wanatumia vema fursa iliyojitokeza ili waweze kuleta mawazo mapya katika tasnia ya uigizaji nchini.








0 comments:

Post a Comment

ufunguzi