Kiongozi
mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen, amekuwa
mwanachama wa kwanza wa kundi la Lord's Resistance Army LRA, kufika
mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake huko The Hague, Bwana Ongwen alithibitisha kuwa ndiye, huku akijieleza kuwa ni mwanajeshi wa zamani wa LRA.
Awali mwezi huu alikuwa amezuiliwa nchini Afrika ya kati, miaka kumi tangu ICC ilipotoa ilani ya kumkamata.

0 comments:
Post a Comment