Mahakama kuu ya Kenya
Mahakama Kuu nchini Kenya imesikiliza mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti wa usagaji na kusema kuwa sasa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uasherati wanaweza kusajili mashirika yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutetea haki zao za kibinadamu.
Majaji watatu wa mahakama hiyo wameiamuru Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kulitambua na kulisajili shirika moja ambalo awali mahakama hiyo ilizuia lisisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini. Majaji ambao walikuwa wanasikiliza utetezi huo ni Isaac Lenaola, Mumbi Ngungi na George Odunga majaji hao wamedai kuwa, katiba ndiyo suluhisho ya kila kitu nchini Kenya na kwamba serikali haitakiwi kuzingatia mafundisho ya kidini katika maamuzi yake ambayo kwa mujibu wa majaji hao, maamuzi hayo yananyima kundi fulani la watu uhuru wao.
Uamuzi huo umechukuliwa huku mashinikizo ya nchi za Magharibi dhidi ya nchi za Afrika ya kuzitaka zitambue rasmi vitendo hivyo vichafu yakizidi kupamba moto. Nchi hizo za Magharibi zimetishia kuzinyima misaada nchi za Afrika iwapo hazitatambua rasmi vitendo vya ulawiti na usagaji.
0 comments:
Post a Comment