![]() |
![]() |
Nimeanza kwa kutoa pole maana mimi nakufahamu, Nimeongea nawe, nimecheka nawe, nimesafiri nawe na nimekula pamoja nawe na nakumbuka ulivyonikaribisha sigara kwa lugha ya kisukuma... mimi nikacheka nikakujibu situmii baada ya kuelewa fasiri ya maneno yako.
Katika mazungumzo yetu nilijifunza jambo ambalo kama kijana huenda ni somo kwa wengine, kiufupi ulinipitisha katika safari yako ya kutoka Mwanza-Tanga hadi Dar hiyo ilikuwa mwaka 1957.
Ilikuwa hivi, wakati nchi yetu kuelekea kupata uhuru kamili serikali ya waafrika ikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilitoa tangazo la kubuni nembo ya taifa kwa mtanzania yeyote na atakayebuni na mchoro wake kutumiwa kama nembo atapewa zawadi.
Michoro miwili ilibahatika kuonekana bora, mchoro wa Ngosha na mchoro wa Seif ,na hapa ndipo safari ya ndugu yetu Ngosha ilianza kutoka Mwanza kuelekea tanga baada ya kupokea wito wa kuhudhuria mkutano wa kuteua nembo ya taifa uliokuwa ukifanyika huko Tanga mwaka 1957.(kwa maelezo yake)
Mkutano baada ya kuzipitia nembo zote nembo ya Ngosha na nembo ya Seif, Ngosha aliibuka kidedea na kutunukiwa zawadi nono,kwa wasiojua ukifanyika hivyo hata kwa aliyebuni jina TANZANIA, Baada ya hafla hiyo.
Ngosha hakurudi kwao mwanza alianza safari ya kuelekea DAR kufanya biashara, na alifanikiwa kufanya biashara na kuishi vizuri, japo Katika maisha kuna ajali nyingi anasema baada ya biashara kukaa vizuri alianza mahusiano na hapo ndio chanzo cha yeye kuanguka kimaisha.
Baada ya kutendwa aliamua kurudi katika fani yake ya uchoraji,.
Kwa Sasa ni mzee na kwa kweli anahitaji msaada ili apone.
Nilichojifunza tukifanikiwa tukumbuke kurejea nyumbani.


0 comments:
Post a Comment