Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka ya moyoni baada ya kuguswa na wimbo wa msanii mkongwe Rehema Chalamile 'Ray C' uitwao 'Unanimaliza.
Kigwangalla amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii instagramu kwa kusema amefurahishwa na kuvutiwa sana kwa jitihada anazozifanya Ray C katika kazi zake za muziki hasa wimbo wake mpya wa 'unanimaliza' hivyo ameona amuunge mkono.
"Mimi kama Naibu Waziri wa mambo ya wanawake, kama balozi wa wanawake na kama daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada Ray C nimeguswa na wimbo wake wa 'Unanimaliza'. Hakuna aliyekamilika sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka na kwa hakika tunahitaji 'a second chance' kila siku za maisha yetu. Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka.. 'With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing!'. Ameandika Kigwangalla
Pamoja na hayo, Kigwangalla amewaomba wadau wote ambao wamekuwa pamoja na msanii huyo siku zote kumpa ushirikiano zaidi kuliko walivyokuwa wanampo hapo awali.
Mbali na hilo msanii huyo Ray na yeye aliweza kushukuru na kusema ametiwa faraja sana na kiongozi huyo 'Heshima kwako Mheshimiwa, nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja baba" alisema Ray C
0 comments:
Post a Comment