,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, March 9, 2017


Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa amekiri kwamba klabu hiyo inadaiwa na aliekuwa kocha wa klabu hiyo na baadae kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Hans va der Pluilm raia wa Uholanzi.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkwasa amesema uongozi wa klabu ya yanga unasubiri Hans awasilishe kiiasi cha fedha ambacho anaidai klabu ya Yanga ili klabu hiyo iweze kumlipa fedha zake.

Mkwasa amesema Yanga imepita katika mchakato wa kupunguza baadhi ya watu waliokuwa wakihudumu katika klabu hiyo kama sehemu ya kubana matumizi kama ambavyo makampuni mengi hufanya, lakini hilo halimaanishi kwamba klabu hiyo ina ukata wa fedha.

Katika hatua nyingine Kocha Msaidizi wa klabu ya Yanga mwalimu Juma Mwambusi amesema kikosi chake kipo katika hari ya kupata matokeo katika mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya zanaco katika ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya mtoano.


Kocha Mwambusi amesema kikosi chake kinakabiliwa na baadhi ya wanandinga ambao wanaweza kuukosa mchezo wa siku ya Jumamosi utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini hana shaka na ushindi kwani ana kikosi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi