,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, March 10, 2017

Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango vipya vya soka vilivyochapishwa na Shiirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA na sasa kufikia nafasi ya 157 mara baada ya kukusanya alama 157, ikiwa ni ongezeko la alama 5 kwani katika viwango vilivyopita ilikuwa na alama 152 na kkushika nafasi ya 158 kwa ubora duniani.

Afisa Habari wa klabu ya TFF Alfred Lucas amesema ili Tanzania iweze kupanda zaidi katika viwango vya soka duniani ni lazima michezo mbalimbali ya kimataifa ipatikane.
Kwa upande wa mataifa mengine yaliyopo katika ukanda wa Afrika Mashariki Uganda inaendelea kushika usukani katika ukanda huo ikiwa inashikilia nafasi ya 74 duniani, na kwa upande wa bara la Afrika inashika nafasi ya 16.
Kenya inashika nafasi ya ya 21 kwa bara la Afrika na nafasi ya 88 duniani wakati Rwanda inashika nafasi ya 24 Afrika na 93.
Burundi inashika nafasi ya 41 Afrika na 139 duniani.
Wakati huo huo Misri imeendelea kuwa kinara kwa kukwea kwa nafasi mbili zaidi hadi nafasi ya 20 kwa ubora duniani, ikifuatiwa na Senegal iliyopo nafasi ya 28 huku mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi moja hadi nafasi ya 32 duniani.
Kwa upande wa mashirikisho yote ya soka pamoja na vyama duniani, Argentina imeendeleza kushika usukani kwa kumata nafasi ya kwanza, nafasi ya pili imekwwenda kwa Brazil, na nafasi ya tatu imekwenda kwa Ujerumani na nafasi ya tatu imeshikwa na Chile.

Mataifa mengine yenye nguvu katika mchezo wa soka pamoja na nafasi wanazoshika, Ufaransa inashika nafasi ya saba, Hispania kumi, na Uingereza nafasi ya 14.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi