Mwalimu mmoja katika Shule ya Texas (Texas High School) amehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani na kutumia masaa 200 kufanya kazi za kijamii baada ya kukutwa na hatia ya kutoka kimapenzi na wanafunzi wawili wa shule hiyo.Mwalimu huyo aanayefahamika kwa jina la Haeli Noelle Wey (28) alikutwa na hatia hiyo mwezi uliopita kwa kutembea na wanafunzi wawili wote wakiwa na miaka 17 kwa kila mmoja na muda wake ambapo inadaiwa alifanya nao mapenzi zaidi ya mara 10.Ripoti ya Polisi ilisema kuwa mwalimu huyo alianza mahusiano ya kawaida na mwanafunzi wa kwanza na baadae yalizidi wakati wakiwa likizo ambapo mwalimu na familia ya mwanafunzi walipotembea nchi za Afrika.“Mwathirika alisema wakati wakiwa Afrika mahusiano na [Haeli] Wey yalizidi kuwa makubwa zaidi,” ripoti ya Polisi.
Mwanafunzi wa pili alianza nae mahusiano katika kipindi ambacho wanafunzi walikuwa wamekwenda katika mapumziko ya pamoja na baada ya mwalimu huyo kutoka kimapenzi na mwanafunzi alimtumia ujumbe wa kumtaka afute ujumbe wote waliotumiana katika mtandao wa Instagram na asiruhusu mtu yoyote kushika simu yake.
0 comments:
Post a Comment