Baraza la Michezo la Taifa BMT limeandaa tamasha maalum la michezo kwa
wanawake ili kutoa hamasa kwa wanawake kushiriki kwa wasichana na wanawake
katika michezo na uongozi ili kuleta maendeleo katika jamii.
Akizungumza na Blogu ya Jamii Mjumbe wa Baraza la michezo la
taifa Jenifer Mmasi amesema tamasha hilo litakutanisha watu wenye marika
mbalimbali.
Jenifer amesema tamasha hilo litajenga mfumo mzuri wa kumuwezesha
mwanamke kushiriki katika michezo kwa uhuru zaidi.
Katika hatua nyingine Jenifer amewataka wadau mbalimbali wajitokeze ili
kuwezesha tamasha hilo kufanyika kwa kutoa michango ya fedha au kuwezesha
tamasha hilo kwa namna mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment