Leo ningependa kumzungumzia kwa kifupi Mtu anayeitwa William Malecela wengi tunamjua kama Lemutuz_Nation. Huyu jamaa wengi huwa tunamuangalia kwa jicho la kawaida, wengi wetu huwa tunamchukulia kama mtu flani mwenye majigambo na mpenda starehe na anasa hasa wanawake. Kwa siku za mwanzoni iliniwia vigumu sana kuweza kumuelewa Lemutuz kwa kujiuliza maswali Je hizo picha anazopost (instagram) zina manufaa gani kwake binafsi? na zina impact gani kwa jamii iliyomzunguka? kiukweli nilikuwa natumia muda mwingi kumfikiria lakini sukubahatika kupata jibu la moja kwa moja. unajua ni kwa nini? Kwa sababu fikira zangu na mawazo yangu vilimuangalia kwa mtazamo negative..
niliamua kugeuza akili yangu na kumwangalia kwa jicho la kibiashara zaidi hapo ndipo nilipoanza kumuelewa anachokifanya kina faida gani kwake na kwa jamii iliyomzunguka,nikisema faida kwa jamii iliyomzunguka nina maana kuwa watu hasa vijana wanatakiwa wajifunze mengi kupitia kwake na wasimuangalie kwa matazamio ya kawaida.
Kubali au ukatae lakini ukweli ni kwamba jina la Lemutuz limeshageuka na kuwa moja kati ya BRAND kubwa hapa Tanzania na Nje ya Tanzania. kwa sababu Lemutuz ni mmoja kati ya watu wanaofatiliwa sana hasa katika mitandao ya kijamii. na Kinachosababisha atazamwe zaidi ni brand yake.
Kwa wale msio fahamu maana ya neno "Brand" ni kitu kinacho kuunganisha wewe na jamii inayokuzunguka? so Lemutuz kujiita "King of all bongo social network hiyo ndio brand inayomfanya watu wampende na wamfatilie."
Moja ya changamoto kubwa kwa vijana waliopo
makazini,walio katika siasa,muziki na hata makampuni yanayotoa huduma ama
kuzalisha bidhaa mengi hayajui brand! Mfano kijana upo kwenye taaluma ya
habari,siasa,sheria ama muziki,jitafakari wewe hasa brand yako ni nini?kama ni
mwana siasa hakikisha unajua brand yako,je ni ni jinsi unavyojenga
hoja?unavyowasilisha hoja ama?
Lemutuz keshaijua silaha yake inayomuunganisha na jamii yake, Kile kinachofanya watu wakupende hicho ndiyo
Brand yako,je wewe waijua brand yako?
Hivi ndivyo vitu vinafanya brand ya Lemutuz kuwa ya kubwa.
1.Uniqueness(Upekee),Hapa nadhani kutakuwa hakuna ubishi kuwa Lemutuz amekuwa akitumia njia za kitofauti(Kipekee) na wengine katika kujenga brand yake. amekuwa akitumia njia ambayo inamfanya mtu atumie akili kumuelewa na hii imemfanya watu wengi wampende, so ili na wewe brand yako ikuwe katika eneo uliopo unatakiwa uwe wa kipekee,hakikisha hufanani na mtu,ukiwa mwanasiasa tengeneza upekee wa jinsi
unavyoongea kwenye mikutano,vikao rasmi n.k,Mfano Chadema walivyo amua kutumia
gwanda,ilikuwa ni kujibrand kwa sababu hakukuwa na chama
kinachovaa kombati,au mtazame Mwigulu kuna
kipindi alijibrand kwa mavazi ya Ili awe tofauti,au kumbuka upekee wa kampeni
za January Makamba ndani ya CCM zilivyokuwa!
2.Unpredictable(usiwe
mtu wa kutabirika), Lemutuz sio mtu wa kutabirika wala kukaririka. back to his career utakutana na kitu alichokianzisha "STRAIGHT TALK" katika straight talk zake Lemutuz amekuwa akija na mawazo tofauti hata ambayo watu walikuwa hawayategemei na hii kitu inaleta kitu kinachoitwa (EXPECTATION) Watu wengi wameshindwa kumuelezea moja kwa moja Lemutuz kwa sababu ni mtu asiyetabirika.
3.Expectation(Matarajio), ili brand yako izidi kuwa kubwa watu
lazima wawe na matarajio na wewe, Lemutuz tiyari watu wanakuwa na matarajio ya kupata habari na matukio yanayotokea kupitia yeye. Lemutuz amekuwa akitoa taarifa na uchambuzi wa vitu mbali mbali na hii imemuongezea attention ya kutosha kwa jamii iliyomzunguka.
4.Emotion Appeling,hii ilitumiwa sana na wapigania uhuru
kujibrand,walihakikisha katika kila wanapoongea hotuba zao zilikuwa zinaleta
hisia na msisimko kwa watu,njia hii hutumika kwa kuwa na mifano mingi chanya
ama hasi lengo ni kuhakikisha unachokizungumza,kiandika,kionesha kinaleta
hisia, Lemutuz ameitumia sana njia hii hasa katika STRAIGHT TALK zake. zimewavutiwa wengi. njia hii huitwa Emotion appelling ama human
context katika Brandingi.
5.Audince needs and wants,lazima ufahamu walaji wako wanataka nini?wasomaji wako katika
ukurasa wako wa instagram wanapenda nini? Hapa Lemutuz alikaa akafikiria what is trending now? akajua kuwa watu instagram wanapenda maisha ya bata ndio maana akaanza kuja na mfumo wa kupost picha za batani. na alivyoona kuwa jamii imemuelewa akaanza kuja na vitu vingine vya ziada ndio kama tunavyoona straight talk na picha akiwa na wasanii wakubwa sehemu za bata.
Ujumbe wangu
kwako,ili uwe Popular,credible na ufanikiwe
malengo yako,hakikisha unajua "Brand"yako!.
Kabla hujapost
chochote mtandaoni,unaijua brand yako itakayoshawishi mamia walike,waje kushare
,kucomment n.k?...
Written by Frank Movic
Written by Frank Movic
0 comments:
Post a Comment