Yani DED Mkumbo alikamatwa kwa kosa la overspeed. Askari aliyemkamata akataka kumuandikia faini, lakini Mkurugenzi huyo akadinda. Akajitambulisha kuwa yeye ni Afisa wa Usalama wa Taifa, hivyo Askari huyo amruhusu aende. Askari akamwambia hata kama ni Usalama wa taifa ni muhimu kufuata sheria za usalama barabarani.
DED akakasirika. Akaanza kutoa maneno ya "hovyo" kwa Askari huyo. Badae akamtolea bastola na kumtishia kumuua. Askari huyo akawasiliana na wenzake, wakaja kumkamata. Kufikishwa Polisi ndipo ikajukikana kwamba Mkumbo ni DED wa Wilaya ya Mkinga na sio Afisa Usalama wa Taifa kama ilivyodaiwa.
Polisi wakamshikilia jana akalala rumande na leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na Mashtaka Mawili. Moja la kutishia kuua na jingine la usalama barabarani, ambapo ana makosa matano yanayohusiana na usalama barabarani.
Malisa GJ
0 comments:
Post a Comment