Bukombe.
Mganga Mkuu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Dk Aubery Mushi amesema
kifo cha mwanafunzi aliyekutwa nyumba ya kulala wageni Septemba 29,
kimetokana na kubakwa na baadaye kunyongwa.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Dk Mushi alisema uchunguzi umebaini kuwa kabla ya
kunyongwa, mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma kidato cha nne Sekondari ya
Katente, Zainab Salum (18), aliingiliwa kimwili na watu wawili, mmoja
akitumia kondomu na mwingine hakutumia.
Alisema uchunguzi unaonyesha mtu mmoja alimshika miguu na mwingine kumnyonga shingo kwa kutumia mikono baada ya kumbaka. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema wanamshikilia
mwalimu mmoja wa sekondari, anayedaiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi na
mwanafunzi huyo.
Source:- Mwananchi Blog
0 comments:
Post a Comment