Posted by Williammalecela.com on Monday, October 10, 2016
 |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala leo asubuhi amekutana na kufanya mazungumzo na
balozi wa Kenya nchini Tanzania Hon Chirau Mwakwere . Katika mazungumzo
wamekubaliana kudumisha ushirikiano na biashara. Balozi wa kenya amesema
nchini Kenya kula mchele wa Mbeya ni fahari kubwa na unapendwa sana.
Mkuu wa Mkoa amemuomba balozi kuwashawishi wafanyabiashara na
wawekezaji kuja Tanzania husani Mkoa wa Mbeya kuja kuwekeza na kufanya
biashara. |
0 comments:
Post a Comment