Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imewarudisha kazini wafanyakazi wa 31 wa BOT waliofukuzwa kazi Miaka 22 iliyopita.
Dar es Salaam.
Wafanyakazi 31 waliopunguzwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT) miaka 22
iliyopita wanatua ‘mzigoni’ tena baada ya Mahakama ya Rufani
kuwarejesha.
Wafanyakazi
hao walifukuzwa kazi bila kufuata utaratibu wakati Serikali
ilipotekeleza masharti ya upunguzaji wafanyakazi kama njia ya
kurekebisha uchumi.
Wafanyakazi
hao kupitia wakili wao, Barnaba Luguwa wamemwarifu Gavana wa BoT,
Profesa Beno Ndulu kuhusu dhamira yao ya kurejea kazini kuanzia kesho
kufuatia matokeo ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Kiongozi
wa wafanyakazi hao, Samson Magoti amesema wanakusudia kuripoti kazini
Oktoba 11, 2016 ili wakapige kazi baada ya ushindi walioupata katika
kesi iliyoendeshwa kwa miaka 22.
Amesema
uamuzi wa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa katika Shauri la Mapitio
Na. 3 la 2014 lililofunguliwa na BoT dhidi yao unawawezesha kuripoti
kazini baada ya kusota mahakamani kwa miaka 22. Magoti
aliwataja wenzake watakaoripoti kazini kuwa ni Nuhu Msuya, C.B. Fande,
Mbaraka Katundu, Fabian Nguyeje, Omari Hassani, Alfonsi John, Audax
Rugaimukamu, Ally Ndaro na Julius Haule. Wengine ni Hellen Warioba,
Louis Mapunda, Yusufu Bakari, Laila Ntenja, James Chambala, E. Nyamoga,
George Joseph na Simon Mashigasi.
|
Monday, October 10, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment