PPF
YAKABIDHI KADI ZA WOTE SCHEME KWA WANACHAMA WAPYA 395 WA IKWIRIRI MKOANI PWANI
NA MWANDISHI WETU,
IKWIRIRI
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”,
umesajili zaidi ya wanachama 395 huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa
Pwani.
Akizungumza
hivi karibuni na waandishi wa habari wakati wa zoezi la ugawaji wa kadi za uanachama wa PPF kwa wajasiliamali wa Ikwiriri kwenye viwanja
vya Chuo cha Maendeleo, Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya,
alisema, wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika kujiunga na mpango huo
baada ya Kanda Temeke kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko
huo kwani kuna manufaa mengi.
“Tuliwaeleza,
mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa
kama mfumo wa ziada au waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi,
wafugaji, Boda boda na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia kima
cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa
mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.
Akielezea
faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na Huduma
ya Afya kupitia NHIF.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na
mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ya biashara kwa masharti nafuu, mkopo wa elimu, pamoja na fao
la uzeeni, alisema Meneja huyo.
Kuhusu
namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja
Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Mfumo huo una njia rahisi ya
kuwasilisha michango yake, ambayo ni kwa kutumia simu za mikononi ambapo huduma
hii imemrahisishia mjasiriamali kuchangia michango yake popote alipo” Alisema.
Baadhi
ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu
ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha
shughuli zao.
“Mimi
ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya
maendeleo” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mjasiriamali.
Naye
Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na
PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.
|
0 comments:
Post a Comment