Alishawahi kufungwa jela japo haijajulikana alikosa nini, na jina
lake kamili ni Salum Njwope na jina hilo nila babu yake. Yeye ni
mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa mama yake mdogo anasema
Scorpio alipokua akitoka nyumbani usiku saa mbili anamuaga mama yake
mdogo huyo kuwa anakwenda kwenye kazi ya ubaunsa katika club kumbe
mwenzie alikuwa anaenda Buguruni kuibia watu mpaka asubuhi ndio anarudi
nyumbani.
Pia scorpion ashawahi kushiriki katika shindano lililojulikana kama
Dume Challenge kama miaka mitatu iliyopita na aliibuka mshindi. Napia
alianza mafunzo ya kucheza caret tangu akiwa mdogo sana napia ni mtu
mwenye nguvu za kuzaliwa nazo.
Kuna kipindi aliondoka nyumbani kwao kwa muda mrefu mama yake mdogo
anadai alikuwa hajui yuko wapi mpaka baadae aliporudi mwenyewe nyumbani.
Amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mkazi mmoja wa Dar
es Salaam eneo la Buguruni kwa kumng’oa macho katika kitendo
kilichoelezwa kuwa ni wizi wa fedha.

Mkazi
wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama
Scorpion, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu
mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili
Said Mrisho.
Scorpion
alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore
na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Munde Kalombola.
Akisoma
mashitaka hayo, Kalombola alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo
Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala.
Munde
alidai, Njwele aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34
ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote
kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.
Kalombola
alidai kuwa mshitakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu
machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.
Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.
Hakimu
Sachore aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo
itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashitaka
yanayomkabili kutokuwa na dhamana.
0 comments:
Post a Comment