Dar es Salaam.
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo
kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa
kipindi kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo
hicho.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu
ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za
utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu
kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na
kutolinda maadili ya watoto.
“Clouds
tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia
bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya
kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.
Mahojiano
yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi
hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na
yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00.
Source:- Mwananchi Blog
Source:- Mwananchi Blog
0 comments:
Post a Comment