![]() |
Rais
John Magufuli ametoa miezi miwili kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
kupeleka umeme wa megawati 10 katika kiwanda cha vinywaji baridi cha
kampuni ya Bakhresa Products Group kilichopo Mkuranga, Pwani.
Rais amesikitishwa na kitendo cha shirika hilo kutochangamkia fursa hasa katika viwanda ambavyo ndio wateja wao wakubwa.
"Nashindwa
kuelewa hvi hawa Tanesco watawezaje kufanya biashara kama hawataki
kuwafikia wateja wao. Nataka kufikia Disemba mwaka huu umeme uwe umefika
hapa," amesema.
Amelitaka
shirika hilo kutambua kipaumbele cha Taifa ambacho ni kuwa ni uchumi wa
viwanda. Amesema viwanda vinahitaji umeme wa kutosha kwasababu
vinasaidia kuzalisha ajira.
Source:- Mwananchi Blog

0 comments:
Post a Comment