Akizungumza na Za Motomoto News, Shamsa alisema maisha ya ndoa ni matamu na anajiuliza na kujilaumu kwa nini alichelewa, hivyo anamshukuru Mungu kwa kumpa Chidi Mapenzi, kwani ni ndoto yake ya muda mrefu ya kupata mume bora ili wajenge familia bora.
“Ndoa ni tamu sana jamani kuliko maisha ya kuwa singo, najiuliza sijui nilikuwa nachelewa wapi kuingia humu, naamini tutaendelea kupendana na mume wangu hivihivi mpaka mwisho wa maisha yetu kwani kabla ya kuoana tulikaa kwenye uchumba kwa muda wa miezi nane na tabia zetu tukaona zinaenda,” alisema
0 comments:
Post a Comment