DIAMOND NA RAYVANNY WAMETISHA KATIKA NGOMA YAO MPYA!!!
Ngoma hiyo ambayo ina matoleo mawili tofauti moja likiwa na mahadhi ya kiasili na lingine likiwa na midundo ya kukata na shoka ya kuchezeka klabu. Ikienda kwa jina la “Salome” ngoma hiyo imetungwa na mkali Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny kutoka kwenye nyimbo halisi “Maria Salome” iliyoimbwa na mwana dada Saida Karoli. Saida Karoli mwenyewe amewakibali Wasafi kwa hii.
Kama bado hudownload ngoma hii, bofya hapa uipate moja kwa moja toka Mkito http://bit.ly/Diamond_
Biti ya nyimbo hii imeundwa na Prodyuza Leizer wa Wasafi Records. Video yake imetengenezwa hapa hapa Tanzania ikiongozwa na Director Nicorux kutoka Afrika Kusini. Tazama video hii hapa: https://www.youtube.com/
Said
0 comments:
Post a Comment