UPANDE
wa Jamhuri leo umetoa majibu ya hoja ya kutaka kufutiwa mashtaka ya
mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita
na mfanyabiashara Revocatus Muyela.
Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.
Mtuhumiwa Miriam Mrita akiwa na askari magereza kuelekea chumba cha kusikiliza kesi inayomkabili.Akijibu
hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana
Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa
haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka.
Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu.
Mtuhumiwa, Revocatus Muyela baada ya kutoka mahakamani.Awali
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada
Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muyela,
walimuua kwa kumchinja dada wa bilionea Msuya, Anathe Msuya.
Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.

Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment