
Awaomba wananchi kutoa ushirikiano na ushahidi bila woga ktk kesi za ubakaji na ulawiti kwa watotoAsema elimu na hamasa vitasaidia kupunguza matukio YA ubakaji na ulawiti kwa watoto

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo amefungua vituo viwili vya dawati la jinsia na watoto na kulipongeza jeshi la polisi na wahisani unicef kwa kujenga vituo hivyo mkoa wa Mbeya 

Hayo ameyasema leo katika hafla YA ufunguzi wa vituo hivyo kituo kikuu cha polisi na kituo cha polisi Ilomba na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kutoa ushahidi bila woga kwa kesi za ubakaji na ulawiti

Amesema takwimu alizonazo mwaka 2013 ktk kesi 1066 ni kesi 159 tu ndizo zilizoshinda, mwaka 2014 kesi 960 ni kesi 259 zilishinda na mwaka 2015 kati ya kesi 1,281 ni kesi 350 tu zilishinda . Kwa takwimu hizo inaonyesha watu hawafiki mahakamani kutoa ushahidi na baadhi YA watuhumiwa kumaliza kesi nje YA mahakama

Amewaomba wananchi na viongozi wa dini na kisiasa kutoa elimu na kukemea kwa nguvu zote matendo YA unysnyasaji kijinsia na ukatibu kwa watoto





0 comments:
Post a Comment