Mbunge wa Viti
Maalum Arusha (CCM), Catherine Magige ‘Cathy’ kufunguka mazito na
kukanusha kuhusu madai yaliyotapakaa jijini Arusha kwamba, amewahi kuwa
na uhusiano wa kimapenzi na mkuu wa mkoa (jina tunalihifadhi kwa kuwa
hakupatikana hewani).
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo
makini kilichopo mkoani humo kimedai kuwa, mbunge huyo yupo kwenye bifu
zito na mkuu huyo wa mkoa kiasi cha kila mmoja kumuundia zengwe
mwenzake ili aweze kuchafuka kisiasa kama si kuharibiana kazi. “Ubuyu wa
motomoto ndiyo huo mimi nakupa, Arusha kwa sasa kila mtu anajua kwamba
Cathy na mkuu wa mkoa haziivi, yaani ni kama paka na panya. Unajua iko
hivi, wale inadaiwa walikuwa wapenzi, sasa kama unavyojua tena mambo ya
mapenzi, ilifika mahali nasikia wakamwagana.
WAKAWA MAADUI
“Baada
ya kumwagana ndipo hapo wakageuka maadui. Wakaanza kuwindana, kila mtu
anamuwinda mwenzake kivyake. Mkuu wa mkoa akatumia mbinu zake kumchafua
Cathy lakini Cathy naye akawa halali, anajibu mashambulizi katika namna
ambayo naye aliona inafaa,” kilidai chanzo hicho.
YADAIWA CATHY ALIMJERUHI
Chanzo
kikazidi kumwaga ubuyu kuwa, mvutano kati ya wawili hao ulizaa matunda
kwa Cathy kwani alifanikiwa kumchongea mkuu huyo wa mkoa kwa wakubwa
wake jambo ambalo lilimuathiri katika majukumu yake ya kazi. “Cathy
alimpiga kombora moja matata
sana mkuu wa mkoa, alichanganyikiwa.
Vita ya mbunge ni kali, alimchoma katika jambo fulani ambalo lilileta
mtafaruku kwa mkuu wa mkoa.
MJADALA NI CATHY, MKUU WA
MKOA “Yaani kwa sasa ukipita kwenye vilinge mbalimbali Arusha stori
inayofukuta ndiyo hiyo. Kuna wengine wanamuunga mkono Cathy na wengine
wanamsapoti mkuu wa mkoa. Lakini kama hiyo haitoshi, waungwana
wanawashauri wamalize tofauti zao maana mabifu hayana maana,” kilidai
chanzo hicho.
ILIANZIA KWENYE UCHAGUZI MKUU ULIOPITA
Chanzo
kilizidi kumwaga data kuwa, ishu ya mbunge huyo kudaiwa kutembea na
mkuu huyo wa mkoa ilianza kwenye uchaguzi mkuu uliopita wakati ambao
Cathy alikuwa kwenye harakati za ndani ya chama kutetea nafasi yake ya
Ubunge wa Viti Maalum. “Kipindi hicho ndiyo watu wanasema penzi la Cathy
na mkuu wa mkoa lilishamiri kwelikweli. Wengi walikuwa wanajua hilo,
nashangaa nyinyi Global mlikuwa kimya kuripoti ishu hiyo,” kilidai
chanzo hicho.
CATHY HUYU HAPA Akizungumza na Risasi
Jumamosi juzi kwa njia ya simu kwa takriban dakika 11, Cathy alikiri
kuzisikia tuhuma hizo ambapo zilianza kupikwa kipindi cha uchaguzi mkuu
uliopita na wapinzani wake kisiasa ili kumchafua na hakuna ukweli wowote
kuhusu yeye kutembea na mkuu huyo wa mkoa.
LOWASSA
ATAJWA “Sikia iko hivi; kwanza unapaswa utambue hayo mambo yalianza
tangu kipindi kile cha kampeni za uchaguzi mkuu uliopita. Hakuna kitu
kama hicho, sijawahi kutembea na huyo mkuu wa mkoa na hakuna kitu kama
hicho.”
KAMPENI ZILIKUWA NGUMU
“Mimi kampeni
yangu nilifanya katika mazingira magumu sana. Kumbuka Arusha yote
ilikuwa ni Lowassa na kulikuwa na watu wake walikuwa wagombee na mimi.
Nimegombea na watu wake ndani ya CCM. “Siku mbili kabla ya uchaguzi,
nilikuwa Marekani kwenye sherehe ya Watanzania, alikuwepo rais Kikwete
(Jakaya) na Membe (Benard), nikawa nimepiga picha na Membe. Wakaigoogle
kwenye mtandao, waliituma kwa wapiga kura wote kunichafua, ile picha
siku mbili kabla ya uchaguzi ilisambaa na ujumbe usemao; huyu ni mtu wa
Membe nini?”
MAKUNDI YA URAIS YATAJWA
“Ni
makundi tu ya urais. Na mimi siku ya uchaguzi watu wa Lowassa walikuja
kwa kishindo lakini namshukuru Mungu uchaguzi ulitendewa haki na mimi
nikawa namba moja, ndipo hapo walipoanza kusuka hayo mambo. “Baada ya
ushindi watu walianza kusema mimi na huyo mkuu wa mkoa tunatoka.
Ukiwaambia leteni ushahidi, hawana. Kwanza mimi siwezi kufanya kitu kama
hicho. Mimi ni mke wa mtu jamani. Hayo ni mambo tu ya siasa wanaleta
ili kunichafua, namshukuru Mungu wameshindwa. “Watu wanashindwa kufanya
kazi na kuleta maendeleo wamekalia kuzushazusha mambo yasiyokuwa na
kichwa wala miguu, mara utasikia hili mara utasikia lile yaani ili mradi
tu wakuchafue,” alimaliza Cathy.
MKUU WA MKOA ATAFUTWA
Ili
kutaka kusikia upande wa pili, mwanahabari wetu alimtafuta mkuu huyo wa
mkoa kupitia namba yake ya simu kwa takriban siku mbili mfululizo
lakini haikuwa hewani ila jitihada za kumtafuta zinaendelea
HABARI NA STORI:ERICK EVARIST/GPL, RISASI JUMAMOSI

0 comments:
Post a Comment