Shirika la afya duniani linataka juhudi kuongezwa katika vita dhidi ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaenea kwa kasi nchini Liberia
huku maelfu ya watu wakiambukizwa upya na idadi hiyo inatarajiwa
kuongezeka katika muda wa wiki tatu zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
Shirika hilo linasema kuwa njia zinazotumika kukabiliana na janga la Ebola hazijafanikisha vita dhidi ya Ebola.
Takriban
watu 2,100 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika
Magharibi hasa katika mataifa ya Guinea, Liberia, Sierra Leone na
Nigeria mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika hilo wahudumu 79 wa afya pia wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Kadhalika shirika hilo limesema kuwa, mashirika yanayopambana na mlipuko wa ugonjwa huo, yanahitajika kuongeza juhudi.
Wakati
huohuo , shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans
Frontieres linasema kuwa limelemewa kabisa na idadi inayozidi kuongezeka
ya wagonjwa wa Ebola nchini Liberia.
Shirika hilo linasema kuwa
kituo chake cha kutoa matibabu mjini Monrovia huwarudisha nyumbani watu
wanaohitaji matibabu kila siku .
Msemaji wa shirika hilo Sophie
Jane Madden aliambia BBC kuwa hali hiyo sasa ni ya vurugu na
isiyodhibitika ambapo ametoa wito wa msaada wa kimataifa.
Mapema
shirika la afya duniani WHO lilionya kuwa Liberia huenda ikashuhudia
maelfu ya visa vya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola majuma
yanayokuja.
Watu 1000 tayari wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi
0 comments:
Post a Comment