Rapa
Joh Makini ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Perfect
Combo' amefunguka na kusema kuwa ile collabo yake pamoja na msanii
Davido kutoka nchini Nigeria anatarajia kuiachia mwishoni wa mwaka huu.
Joh
Makini alisema hayo alipokuwa akichat na mashabiki zake kupitia mtandao
wa 'Facebook' na kusema kama kila jambo litakwenda lilivyopangwa huenda
mwishoni mwa mwaka huu akaachia kazi hiyo ambayo inasubiriwa sana na
mashabiki wake. Kwa upande mwingine msanii Joh Makini alisema collabo
yake na msanii Bongo fleva Alikiba pia inakuja hivyo mashabiki wasitie
shaka juu ya jambo hilo kwani lipo njiani kuja nalo.Pia Joh Makini
alisema kwa sasa lego lake kubwa ni kuona anakuza muziki wa Hip Hop wa
bongo Afrika na duniani kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment