Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Akizungumza na Maafisa mipango miji jijini Dar es salaam leo. Kulia Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa.
WAZIRI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka watendaji wa wizara hiyo kuendelea kujenga nyumba za makazi za watumishi wa serikali mkoani Dodoma.
Akizungumza na maafisa wamipango miji jijini Dar es salaam leo Waziri Lukuvi amewataka watendaji hao kuweza kujipanga kujenga nyumba za makazi za watumishi wa Serikali ilikuweza kuwahudumia watumishi hao wanaotarajia kuhamia mjini Dodoma.
''Lengo la kikao hiki ni kuwataka mjipange ili kuweza kujipanga ni namna gani mtaweza kuhudumia watumishi wa serikali wakati wakiwa mjini Dodoma''amesema Waziri Lukuvi.
Amesema kuwa sambamba na wizara mbalimbali kuhamia katika jiji la Dodoma amewataka watendaji hao kuweza kuboresha ramani ya mipango miji ilikuonesha namna gani mji unavyotakiwa kukaa ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo .
''Tumeshamaliza mastar Plan tangu mwaka 2010 ya Dodoma kwani maeneo mengi yakuishi yameshaainishwa nilazima maafisa mipango kufanya biashara ikiwemo viwanja vyandege.
Nae Katibu wa Wizara hiyo, Michaeli Mwalukasa amesema kuwa serikali inaandaa sera ya nyumba ikiwemo muswada wa uendelezaji miliki katika miji mbalimbali hapa nchini.


0 comments:
Post a Comment