
Msanii
Diamond Platnumz amefunguka na kuwataka wasanii ambao wanachipukia na
wale ambao wapo kwenye muziki wafikiri kufanya mambo zaidi yake na
wasifikirie au kuwaza kuwa kama Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz
alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na
kusema wasanii ambao watakuwa wakimuwaza yeye watakuwa watumwa wake,
lakini kama watafikiria kufanya vitu zaidi yake itasaidia kwani itafanya
kila mtu kuwa na njia yake na kuweza kufanikiwa zaidi katika muziki wao
pamoja na maisha kiujumla.
"Mimi nataka kuwaambia
wasanii wafikirie kufanya vitu vikubwa zaidi wasifikirie kuwa kama
Diamond Platnumz, maana kama watakuwa wanafikiria kuwa kama mimi
watakuwa watumwa wa muziki wangu na maisha yangu, mfano unafikiri Wizkid
angeamua wa 'copy' P Square ingekuwaje? Jibu angekuwa mtumwa wa P
Square lakini kwa kuwa alitoka kivyake vyake ndiyo maana saizi Wizkid
anafanya vizuri zaidi hata ya P Square ulimwenguni" alisema Diamond
Platnumz.
0 comments:
Post a Comment