,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, June 24, 2016

 
Mmiliki wa gazeti la DIRA ya Mtanzania Alex Msama, amemwomba radhi Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe kwa gazeti lake kuchapisha habari mbili ambazo hazikuwa na usahihi.Alex Msama ambaye ndiye mmiliki wa gazeti hilo ambalo limejikuta matatani siku za hivi karibu baada ya kuandika habari zinazoelezwa kutokuwa na usahihi, amemtaka radhi Waziri huyo ambaye alisema atakwenda mahakamani kulishtaki gazeti hilo kwa tuhuma za kuandika habari zinazomuhusu ambazo alidai hazina ukweli wowote.
Gazeti la DIRA lilichapisha habari yenye kichwa cha habari kinachosomeka “Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani” huku habari nyingine ikisomeka “Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2” ambazo zote zinaelezwa kuwa ni za uongo.
Msama alisema kuwa habari hizo hazikufuata taratibu za uandishi na katika kuhakikisha analeta ufanisi amemsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo Mussa Mkama kwa tuhuma za kuhusika na uchapaji wa habari hizo zilizokiuka misingi ya uandishi.



 
Mussa Mkama.
Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.
Msama alikaririwa akisema “Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni.”
Aidha kuonyesha amekerwa na taarifa hiyo, ameahidi kuchapisha habari ukurasa wa mbele wa gazeti hilo kuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Ukiachia mbali salata la Dkt Mwakyembe, gazeti hilo limejikuta matatani kwa mara nyingine baada ya kudaiwa kuandika taarifa ya uongo kuhusu kuibwa kwa kifaru cha jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ).
JWTZ ilitangaza kuchukua hatua kali kufatia kupotoshwa huko kwa ukweli

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi