,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, December 30, 2015



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watumishi wa wizara hiyo katika kitengo cha huduma kwa wateja, kufanya kazi hadi usiku ili
 

kuhakikisha wanawahudumia kwa muda wananchi wengi wanaofika katika kitengo hicho na kuondoka bila kupata huduma stahiki.

Waziri Lukuvi alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kitengo hicho na kubaini kuwepo urasimu mkubwa unaopelekea wananchi kushindwa kupata huduma kwa wakati. 
Baada ya kuzungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kitengo hicho, alibaini kuwepo wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia hati zao kwa takribani miezi mitatu bila mafanikio lakini alipoagiza wapewe hati hizo zilipatikana mara moja.

“Watu wasirudi bila kuhudumiwa. Na kama ni wafanyakazi watabaki mpaka usiku, tutafanya utaratibu wa hao wafanyakazi wanaobaki mpaka usiku. Wafanyakazi wabaki muda zaidi lakini kila anayekuja katika kituo kile lazima ahudumiwe,” alisema Lukuvi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi