Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr. |
Kocha
Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa anaweza
kutimuliwa ndani ya kikosi hicho na nafasi yake kupewa kocha wa zamani
wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovoc, ameibuka na kusema suala hilo
wala halimtishi hata kidogo.....,
Hivi
karibuni kuliibuka taarifa za ndani ya Simba zikisema uongozi umempa
Muingereza huyo michezo ya mzunguko wa kwanza iliyobakia kuhakikisha
anapata matokeo mazuri la sivyo anaweza kuondolewa kukioongoza kikosi
hicho.
Kerr alisema anachojiamini ni kwamba kazi yake anaifanya ipasavyo hivyo hata akitimuliwa ni kama wanamuonea tu.
"Hilo
suala la kuondolewa wala halinitishi hata kidogo, nimekuwa nikiifanya
kazi yangu kwa ufanisi lakini mazingira yanatunyima kufanikiwa na kupata
ushindi.
"Kabla
ya mechi yetu na Mwadui tulikua tukifanya mazoezi kwenye uwanja mbovu
ambao ni kama sehemu ya malisho ya ng'ombe, kocha unatakiwa kuiandaa
timu katika hali nzuri ili mpate matokeo mazuri. Pia siku moja kabla ya
mechi tulikwenda uwanjani tukaukuta haupo katika kiwango kizuri.
"Binafsi
hata mimi matokeo haya yananiumiza, mashabiki wengi kutoka Dar walikuja
kutusapoti lakini wameondoka vichwa chini, baada ya mchezo nilimuona
mwanadada akilia kwa uchungu kisa hatujapata ushindi, hiyo inaonyesha ni
jinsi gani mashabiki wanaumizwa na matokeo mabaya," alisema Kerr.
Sare
iliyoipata Simba, juzi Jumamosi ni ya tatu mfululizo, ilianza kutoka
sare ya 2-2 dhidi ya Azam kisha ikaambulia 1-1 na Toto Africans.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment