,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, December 30, 2015


 

Wizara ya Maliasili na Utalii, Tamisemi na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano inategemea kuanzisha programu ya pamoja wa upandaji miti nchini kwa ajili ya uhifadhi na undelezaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja uliwakutanisha
Mawaziri wa Wizara ya Maliasili, Utalii na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na
Muungano na jopo la wataalamu, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne
Maghembe amesema Serikali ya awamu ya tano imekusudia kuboresha uhifadhi wa
mazingira.

Prof. Maghembe. Ameongeza kuwa Wizara
ina maeneo makubwa yaliyotengwa kwa ajili ya kupanda miti ili kuzuia uharibifu
wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuzuia ukataji miti hali inayotishia nchi kuwa
jangwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa mapema.
‘’Tupo tayari tumejiandaa na tunaweza
ikiwa nia yetu ni kuhakikisha nchi nzima inapandwa miti kwa wingi na kwa
usimamizi wa hali ya juu kwa kuwashirikisha wananchi’’ Prof. Maghembe
alisisitiza.

Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba ulikuwa na lengo
la kuipa kazi kamati maalum kwa ajili ya kuandaa andiko maalum litakalotumika
kuandaa mpango mkakati huo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba Kamati hiyo imepewa wiki mbili
kuhakikisha inakamilisha kazi hiyo ambapo utekelezaji wake unategemewa kuanza
mara moja ukiwa na mbinu mpya zaidi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi